nimeipenda sana hii picha wamependeza pamoja na mtoto wao wakionekana wenye mapenzi mazito na furaha katika maisha yao hakuna asiyetamani kuwa na familia yenye amani na furaha siku zote,lakini unakuta matatizo yanatokea na baadae familia inasambaratika na watoto wakiishi bila ya mama au baba ,ni jambo la kumuomba Mungu uwe na familia borah na amani na furaha vitawale katika maisha yenu.muhimu kutambua furaha katika familia.
Maoni 4 :
wamependeza sana big up adela,furaha ni kila kitu katika mahusiano jamani
wamependeza sana mpendwa wachache sana kuwakuta hivyo katika maisha ya sasa..
ni kweli wamependeza familia ni kitu kizuri sana na ni agizo la mwenyezi mungu kuwa na familia utakumbuka tangia enzi za adamu na hawa inapotokea tofauti ni mazingira tu yamelazimisha
asanteni wapendwa kwa kutembelea blog yangu,ni kweli furaha na amani katika familia inaleta faraja na siku zote tuwe makini kulipigania hili katika familia zetu......
Chapisha Maoni