Jumatatu, Novemba 15, 2010

Katika mapenzi usilalamike kuwa unatendwa vibaya inawezekana wewe ndiyo tatizo,,,tafakari kwanza


Mapenzi ni matamu sana lakini inapotokea migogoro hubadilika na kuwa machungu,kuna baadhi ya watu hususani wanawake wana tabia ya kulalamika kuwa wanatendwa au kuumizwa katika mahusiano huku wakiwa hawatafakari kwa nini anaumizwa inawezekana tatizo likawa kwake lakini kutokana na kushindwa kutafakari kila siku anabaki analalamika na kukata tamaa katika mahusiano


Unatakiwa kuwa na uhusiano ulio huru na furaha wakati wote kwani kulalamika bila kutafuta ufumbuzi wa tatizo haisaidii zaidi inaongeza matatizo

Inawezekana kuwa na uhusiano wa kudumu kwa kujitambua na kujua nini umuhimu wa uhusiano mlionao, husuani yanapotokea matatizo kama migogoro inayotokana na usaliti nk. kuwa muwazi ni hali ambayo mnatakiwa kujijengea wakati wote kila mmoja kuwa muwazi kwa mwenza wake.

Usitake mwenzio akufanyie mazuri wakati wewe haumfanyii mazuri,, KUWA MAKINI USIMPOTEZE UNAYEMPENDA.

Maoni 3 :

Yasinta Ngonyani alisema ...

Adela! umenena mapenzi ni kutendeana si mmoja tu amtendee mwenzie hapana. Ni sawa na ukiwa na rafiki wewe unampigia simu au unamtumia ujumbe lakini yeye wala hajali ...unafika wakati unakata tamaa na urafiki unakufa. kwa hiyo mtendee akutendeaye utaona utamu wake:-)

Bila jina alisema ...

kabisa, ila kuna mijianaume mingine eti umpende tu, umuheshimu, umumie msg asijibu, ukiacha kutuma anauliza oooh mbona cku hz hutui msg nzuri nzuri, he jamani INAHUSUUU....

ney alisema ...

ano namaba 2 nimeipenda hawa wanaume ndio walivyo...ila ndio watoto wetu tufanyaje sasa...

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom