Jumatano, Novemba 24, 2010

Maisha ni kujipanga na si kukurupuka hayo ni maneno kutoka kwa binti Mrembo Aneth Nyoni mtangazaji wa Radio passion na Tumain television

Aneth akiwa katika pozi leo nimezungumza naye akanimbia maneno mazuri sana amesema katika maisha siku zote ukitaka kufaninikiwa usikurupuke jipange kisawasawa na kujituma kwa bidii ili kufikia malengo yako,kuna baadhi ya watu wanafikiri kuwa na maisha mazuri ni kitu ambacho kinakuja haraka bila kufahamu waliowengi wametokea mbali sana hadi kufanikiwa alisisitiza Aneth.
Pia alisema kama ni mwanafunzi umepata nafasi ya kusomeshwa soma kwa bidii, na kama ni mfanyakazi fanya kazi kwa bidii, na kwa yule ambaye hana kazi asijibweteke kwani inawezekana kujiajiri mwenyewe jambo la muhimu tusichague kazi wakati unajua unaishi katika mazingira magumu utaanza maisha kwa tabu lakini baadaye utakuwa juu na kufurahia maisha yako...UJUMBE UMETULIA MAISHA NI KUJIPANGA NA KUWA NA MALENGO.

Maoni 2 :

emu-three alisema ...

Yah ni kweli, kupanga kwa mpangilio, utafanikiwa!

Bila jina alisema ...

Nakubaliana na wewe Adela. Huyu Aneth anaonekana mrembo. Kwenye hizo picha she looks simple but mkali. Ujumbe mzuri, ni wakufanyia kazi.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom