Ujumbe huu ulikuwa unasema,,mimi ni mwanamume nina mke ambaye nimeishi naye kwa miaka minne sasa bila kupata mtoto,mwanzoni mke wangu alikuwa akinisihi tuende hospitali kuangalia tatizo liko wapi lakini mimi nilikuwa nakataa na kumwambia yeye ndiye aende lakini sikuzote alipokuwa akienda alirudi na kuniambia kuwa Daktari alimpa majibu kuwa hana tatizo lolote na kunishauri na mimi niende kiukweli nilikuwa mkali sana kila aliponiambia niende hospitali na ndugu zangu wamekuwa wakimlaumu mke wangu kuwa hazai mimi nampenda sana mke wangu hivi majuzi nilienda hospitali ili kuangalia kama nina tatizo nilifanya hivyo bila kumshirikisha mke wangu majibu niliyoyapata kutoka kwa daktari ni kwamba sina uwezo wa kumpa mimba mwanamke,majibu haya yamenikatisha tamaa kuna wakati natamani kujiua naogopa kumwambia mke wangu naumia sana moyoni najiona kama sistahili kuishi. naomba ushauri nifanyeje.......... |
Maoni 7 :
Yote ni mapenzi ya mungu na msema kweli ni mpenzi wa mungu. Jambo jema kaa na mkeo mwambie ukweli na shaurianeni, natumai kwa kushauriana kwenu mnaweza mkafikia ufumbuzi, kwani wapo hawana matatizo kabisa kwenye kizazi na bado hawati watoto, je hawa watasemaje? Ina maana wakati mwingine kupata ujauzito/mtoto ni mapenzi yake rabana. Msitoke nje ya imani za dini mnapokuwa na mitihani kama hii. Ikibidi ombeni ushauri kwa wakuu wa imani zenu za dini!
Pole sana kaka yote ni mambo ya mungu hayo ila cha msingi usife moyo na usikate tamaa, kaa na mke wako muongelee hili swala na nina imani kubwa sana atakuelewa na ataficha siri yenu ya ndani, si wewe peke yako mbona wako wengi wenye tatizo kama lako? Usikate tamaa na wala usisononeke sana yote ndo mambo ya mungu haya, na pia nenda kwa dakatari kama 2 au 3 usikie watakavyokujibu pia, god bless u.
Je madaktari hawakukuambia kwanini huna uwezo wa kumpa mimba mkeo?kama ni mbegu zako hazina virutubisho vyenye nguvu basi siku hizi kuna dawa za kuongeza nguvu za virutubisho.
Pia siku kuna hospital unakwenda na mkeo anapandikizwa mbegu zako kwa njia ya test tube na anapata ujauzito, sijui kama bongo zipohizo hospital.Dubai na Muscat nchini Oman zipo.gharama ni kubwa kiasi.wasiliana nami nitakupa address yao na uwaulie online.
salehjadeed@hotmail.com
Usijiue kwani we si wa kwanza kuwa na tatizo hilo na hutakuwa wa mwisho. Magonjwa hayo yanatibika kwa dawa na mbegu zinahuishwa na unampa mkeo ujauzito bila tatizo lolote.
Pia ikishindikana hiyo kuna IVF ambapo wewe na mkeo mnaenda mnatoa mambo yenu na mkeo anapandikizwa kijusi na atazaa. Huan haja ya kwenda Oman, Kampala tu happo ipo hospitali inayosaidia sana tu, ntaitafuta linki nimtumie Adela naye atakupa. Tatizo tu ni kwamba ukae a mkeo, umweleae ukweli na pamoja mshirikiane mtoto mtamata. Pili inabidi mzichange maana kidogo haka kaprocedure ka IVF kanahitaji mkwanja. Mwisho mtoto ni zawadi kutoka kwa Mungu kama vile ilivyo zawadi nyingine, huyu anapewa hii yule anapewa ile.
mmmmmh
POLE SANA KAKA YANGU,
ILA TAFADHALI NAKUOMBA ONDOA MAWAZO HAYO YA KUJIUA.HILO TATIZO SIYO LAKO PEKE WATU WENGI WANALO, NA UZURI WAKE KUNA NJIA YA KITAALAM ZAIDI ZITAKAZOKUWEZESHA KUPATA MTOTO,ENDELEA KUWASILIANA NA WATAALAM PAMOJA NA KUFUATA USHAURI WALIOUTOA WENGINE HAPO JUU.
PIA VUNJA UKIMYA ONGEA NA MKEO,NAAMINI UKIONGEA NAYE HAUTAKUWA TENA NA WAZO HILO LA KUJIUA,
POLE SANA.
POLE SANA.
Huyu kaka kama tatizo lake lipo bado awasiliane na mwenye namba hii: +255 715 680 171.
Chapisha Maoni