Habari yako Adela naomba ushauri kupitia blog yako mimi ni mwanamke nimeolewa nina miaka mitatu katika ndoa na mtoto mmoja, Tatizo mume wangu huwa anatabia ya kunipiga sana kila akirudi usiku na wakati mwingine nikimuuliza kwa nini amechelewa kurudi anachukia na kunipiga na hata udiriki kunipiga mbele ya mtoto wetu na kila mara hii hali inajirudia na nikitaka kuondoka analia na kuomba msamaha kuwa ananipenda hatorudia tena kitu ambacho si kweli kwani baada ya hapo zikipita siku mbili ananipiga tena mimi nimechoka nahisi ipo siku ataniua naombeni ushauri |
Maoni 5 :
Kuna mtu mmoja kaniambia makabila mengine `kipigo' ni sehemu ya mapenzi na kama mke hajapigwa atasema mumewe hampendi....lol
Kwanini mtu kama unampenda umpige, umuumize...kweli ndio mapenzi hayo. Ujiulize kama wewe ungepigwa ungefurahi?
Kaa naye ongea naye mueleze nini unapata,..maumivu gani unapata, na umuulize hebeu nijarinbu kukupiga uone kama ina raha...kama haina raha inaumiza sasa kwanini unitendee mimi!
Kama unaweza kuondoka ondoka mwanakwetu!
Unajua mara nyingi ni mtu mwenyewe afundishaye watu jinsi hao watu watakavyo mtendea na watu mara nyingi hufanya kile tu wanachoweza kufanya.
Huyo bwana yako kashagundua anaweza kukupiga na kukukulilia ukamsamehe kwahiyo:
Unafikiri kwanini awe na sababu yakuacha tabia hiyo wakati anajua inawezekana?
Tatizo kubwa mna MTOTO ,...
... ila mtoto anayeshuhudia kila siku mama yake akipigwa ukiendelea kumuweka katika mazingira hayo unamuaribu huyo mtoto kwa kuwa kwanza KISAIKOLOJIA mnamuumiza na maugomvi yenu ambayo MTOTO hawezi kuyaelewa na watoto wanaoathirika kihivyo wanaweza kuwa WATU WAZIMA wenye matatizo sana tu!
Mimi naona ondoka,...
.... akijua una maanisha atakutafuta na wakati kakufuata wewe utakuwa katika nafasi nzuri ya kutawala ni unataka kwenye mahusiano yenu.
Ni mtazamo tu HUU hasa nikiamini mara nyingi kuna pande mbili katika kila stori!
Usipoteze muda kuongea naye, na hakuna pande mbili wala tatu. Hata kama unamuudhi hana HAKI ya kukupiga! Inaumiza sana wanawake mnapigwa tena mbele ya watotot wenu! Hapo ushamtesa na mwanao pia. Ondoka pleeeeease! Mwanaume anayekupenda hakupigi hata siku moja. Usipoangalia utaacha mtoto wako yatima. na yatima wanateseka rafiki yangu usipime. Run, for ur life, run. hakuna discussion. mwache akatafute bondia mwenzie. Pole sana. Ondoka na umrudie Mungu wako, atakuonyesha mambo makubwa magumu usiyoyajua!
MAMA NO LOVE THERE,TAKA YOUR TIME
dada yangu ondoka hapo hapakufahi hata akikulilia machozi ya damu mwache kimbia wala usigehuke nyuma plz hondoka maisha yako ndo bora kuliko chozi lake lakinafiki.
Chapisha Maoni