Habari yako Adela mimi ni mwanamke nimeolewa, katika mahusiano yetu na mume wangu kabla ya kufunga ndoa hakuwahi kuniambia kama ana watoto na tumekuwa katika mahusiano takribani miaka miwili baada ya kunioa kwa sasa nina mwaka mmoja katika ndoa yangu mume wangu ameleta watoto watatu na kunitambulisha kuwa ni watoto wake na anataka waishi hapa nyumbani na mimi kwa sasa ni mjamzito kiukweli roho inaniuma sana sikuwahi kufikiria kama ingekuwa hivi kwani hata nikimuuliza yeye ananijibu kwa kiburi kuwa watoto ni wake na akiamua anaweza kuleta watoto hata kumi ,,nafsi yangu inaumia sana na sijui nini hatma ya uhusiano wetu kwani hata mama wa hao watoto simfahamu na mume wangu nikimuuliza anasema hayanihusu. watoto hao mkubwa ana miaka 11, wa pili mika 7 na mdogo miaka 4. naombeni ushauri nifanyeje
Maoni 3 :
huyo kaka ni selfish,kukuficha jambo kubwa kama hilo la kuwa na watoto.na majibu ya ujeuri juu.huyo kaka atakuja kukusumbua baadae.mmh hao alioachana nao inaonyesha yaliwashinda,be careful inasikitisha kwani ndoa bado changa.jaribu kufocus na mimba yako,hao watoto hawana makosa,kosa ni la huyo baba.wasiwasi wangu hayo majibu yake yanaweza kusababisha ugomvi wa mara kwa mara.na asije akawa viburi hao watoto.kaa nae kiupole mfahamishe how you feel,na hao watoto kaa nao vizuri
Lea tu hao watoto wala usijae pressure bure maadamu uliolewa naye huna budi kuyaoga,muhimu ni kutuliza moyo basi.Ukisema utoke hapo ni kujiletea matatizo.Ila ni vema umjue mama yao na kama kuna uhusiano unaendelea au vipi.Kukaa na watoto si hoja maadamu yeye ndiye mtoa matunzo yao lisikupe shida hilo.
nnachokuomba tu we dada mme wako ndio anamakosa tena makubwa tu ya kutokuambia kama ana watoto mimi ninachokuomba tu usije tesa hivyo viumber vya watu maana hawana makosa wala usiwanyanyase.
Chapisha Maoni