Ijumaa, Aprili 01, 2011

Mpenzi wangu anapenda sana kunikumbusha wapenzi wangu wa zamani na anataka niwe nawapigia simu mbele yake simuelewi jamani...

Ujumbe huu nimeupata kutoka kwa mdau hakutaja jina lake  Nisaidieni mwenzenu sijui nifanyeje. Mimi na mpenzi wangu tunapendana sana. Siku moja kila mmoja wetu akawa anamweleza mwenzie historia ya maisha yake, na marafiki ambao amewahi kuwa nao. yeye aliwahi kuwa na girl friend, na mimi niliwahi kuwa na boy friend ambaye kwa sasa sina mahusiano naye tena.Huyu mpenzi wangu ananiambia amekata uhusiano wa kimapenzi na wale wa zamani pamoja na kwamba wanapigiana simu. Kinachonikera yeye hupenda sana kunikumbushia wapenzi wangu wa zamani, na kutaka niwapigie simu mbele yake, tukiwa mahali wakati wa kuachana ananiambia msalimie mpenzi wako fulani. Kwa kweli ninakereka sana. hata nikimwambia hii inaniudhi haachi.Hii inanifanya nakosa kabisa hamu ya mapenzi hata wakati ninapokuwa namhitaji. Upendo unazidi kushuka Nifanyeje?


Maoni 2 :

juliusmbalwa alisema ...

adela hapa hakuna mapenz kuna ulazima gan kujva mahusiano ya zaman ya mpnz wako?wa kaz gan?huyo men ana wivu mkubwa tena wa hatar alimtega amjue tabia za huyo dem na wanapoagana anapo mwambia msalimie bwn wako yan anamchukulia huyo dem kama malaya.wajua mwanaume hapend kujua dem wake katoka na watu wangap anajihs pengne hao wa zaman walikuwa wanajua mapenz sn na v2 kama hvyo

Bila jina alisema ...

Ni njia ya kukufukuzia hiyo kaa ukijua kuwa anataka kukuudhi ili umkimbie kia aina hivi.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom