Kutokana na kura zilizopigwa imeonekana wanaume ndiyo wanaongoza kwa usaliti katika mahusiano kwa 46% ikifuatiwa na walio kwenye ndoa kwa 26% na 23% ikiwa ni wanawake na mwisho ni asilimia 3 kwa wote,, kiukweli mimi naweza kusema kwamba tatizo la usaliti katika mapenzi linaweza kuwa la wote lakini wanaoongoza wakiwa ni wanaume kama ilivyoonekana but ni nini hasa kinapelekea wanaume kuongoza sana katika hili suala la kutokuwa mwaminifu katika mahusiano??.................. |
Maoni 3 :
Swala zima la uaminifu katika MAHUSIANO ni JIPYA!
Inatakiwa mtu uangalie MAHUSIANO ni nini kwanza na ni lini kiitwacho MAHUSIANO kionekanacho sasa hivi cha MWANAMUME mmoja na mwanamke mmoja kilianza kukubalika kuwa ndio sahihi.
Ukifuatilia utagundua MWANAUME hasa kwa kuwa sio apataye MIMBA tokea enzi za hakuna kondomu wala dawa za kinga za mimba alikuwa na uhuru zaidi wa kuwa na mahusiano na wanawake wengi bila kuhofia kitu kitu kilichofanya watoto wa kiume waachiwe huru na wasichana ambao wanaweza kupata mimba na kutia aibu familia wachungwe.Kitu kiendeleacho kufanya watoto wa kiume kuwa huru zaidi katika maswala ya mahusiano ya mdhaha kuliko wasichana.
Wavulana walikuwa ndio wenye misuli ya ULINZI wa jamii waishiyo na watafutaji wakuu wa msosi wa jamii wa uhakika mwaka mzima ukizingatia mwanamke kuna wakati fulani wa ujauzito kuna mengi hawezi na walikuwa wanakufa sana wakati wa kujifungua . Kitu kilichofanya wanaume wawe na wanawake zaidi ya mmoja just in case.
Morality za Mwanamume awe na mwanamke mmoja ni mpya na nizakujifunza tu juzijuzi na ulizi wake uko kwa KISAIKOLOJIA tu bado kwa kuwa BAOLOJIA haisapoti mahusiano kihivyo.
Kabla ya yote unatakiwa uangalie tofauti za MWANAUME na MWANAMKE kibaolojia mpaka kisaikolojia huku ukifuatilia historia za watu kuanzia kiupataji wa mlo kujilinda nk. - ili kuweza kuona ni kwanini kuna wadaio WANAUME ndio wazidio kiusaliti wa mahusiano kitu ambacho pia kwa siku hizi huweza kuwa sio kweli.
Kwa kifupi :
Mwanaume kikuathirika ,..
.... anazurika kidogo HISTORICALLY kwa kuwa msaliti kuliko MWANAMKE ambaye kirahisi UMALAYA wake utaonekana mbaya kuliko mwanaume akiwa kitombi!:-(
Samahani kwa kupapasa wazo kiharakaharaka!
:-(
asante sana Simon kwa ujumbe huo tuko pamoja naamini mdau atakuwa amepata kitu fulani kutoka kwako.But mi naamini inawezekana kuwa muaminifu haijalishi ni mwanamke au mwanamume muhimu kujitambua na kuwa muaminifu wakati wote
Nyongeza Fikirishi.
Biblia nayo inaeleza mwanzo wa dhambi kwamba; Eva (Hawa) alipoachana na Adam kwa muda kidogo tu shetani akapata nafasi ya kumrubuni.
Fuatilia kitabu cha mwanzo katika Biblia. Mengine yote ni mitizamo tu.
Chapisha Maoni