Jumatano, Mei 04, 2011

Hisia za kuumizwa katika mapenzi kwa mwanaume hazitofautiani na za mwanamke,,wote wanaumia

Katika mapenzi kwa asilimia kubwa wanawake huwa wanaona wenyewe ndiyo wanaumia sana linapotokea  suala la usaliti katika mahusiano aliyonayo, lakini ni wazi kabisa hata wanaume wanaumia sana kwahiyo usifikiri mwanamume akisalitiwa hawezi kuumia hapana kwani hata yeye ni binadamu inapotokea ametendwa basi lazima ataumia ijapokuwa maumivu yanatofautiana,, mwanamke anaweza kuonyesha wazi maumivu anayoyapata lakini mwanamume akawa anaumia moyoni huku akijionyesha usoni kuwa hajaumia kumbe anaumia sana. kwahiyo naweza kusema maumivu ya mapenzi hayaangalii mwanamume au mwanamke inategemea na wewe ulipenda kwa kiasi gani.

maumivu haya hutokana na vitu vingi ikiwemo kukosa uaminifu, kuachana au kuachika nk,,na kutokana na maumivu haya hupelekea baadhi ya watu kujuta kupenda,, kuapa kutopenda tena,,na hata kunywa sumu na kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi. Muhimu ni kuzingatia suala la mapenzi ya dhati na kuishinda tamaa,,hakuna anayependa kuumia katika mapenzi kwahiyo basi kama hupendi kuumizwa usimuumize pia mwenzio,,,kwasababu kuna wengine ni mahodari kuwaliza wenzi wao kila kukicha. Tubadilike jamani mimi naamini hakuna kinachoshindikana

Maoni 3 :

miram3.com alisema ...

Kusalitiana ni kuvunja mkataba wa ndoa. Na tukumbuke kuwa ndoa ni nusu ya dini. Na dini ni mafungamano kati ya mja na mola wake! Angalia utakatifu wa ndoa ulivyo!

Simon Kitururu alisema ...

Wote tunaumia na sio katika mapenzi tu!

Ila kwa mtazamo wangu kinachosahauliwa BINADAMU hawaumii sawa hasa ukizingatia kuwa BINADAMU tunatofautiana katika kuyapa maana MAUMIVU!

Na apataye maana fulani kimaisha hatafsiri kuumia sawa na aumiaye tu na maumivu yake hayana maana fulani!
Kwa mfano:


Kuna imani nyingi hasa za ASIA ambazo moja ya wafanyayo kiuaminifu na KIIMANI ni kujiumiza. Kwa mfano Waislamu wa SHIA mpaka IRAKI wakakatazwa na Saddam Husein kujikatakata mapanga kwa kuwa wanamchezo KIIMANI kujikatakata wakimkumbuka mmoja wa ndugu ya Mtume Mohamed ambaye aliuawa hapo Iraki ambaye ndiye miongoni mwa waheshimiwao na WASHIA. Na wale maumivu yao yanamaana na kutokwa kwao madamu kuna maana na ni faraja kwao kusikia hayo maaumivu na kwa hiyo MAUMIVU yao ni tofauti na ukimchukua Muislamu wa dhehebu la SUNNI ambaye haamini hilo ukamwambia ajikatekate asikie maumivu. Maumivu yake yatakuwa zaidi.

Au niseme kuna wakati nilikuwa siamini kuwa ni kweli kuna watu MAUMIVU hata ya kupigwa na mpenzi ni moja ya wakitafsiricho kama PENZI. Na ni mpaka nilipokutana na wasichana wakiricho hicho TANZANIA na hata UGHAIBUNI ndio nikakubali kuwa katika MAUMIVU inategemea yana maana gani kwako. Ingia SEX SHOP lolote ULAYA utakuta vifa vya kutiana maumivu vinauzwa. Na haki ya nani nishakutana na binti wa Kitanzania miaka kadhaa iliyopita ambaye nafikiri Kisaikolojia kutokana na kuona BIBI anapigwa , MAMA anapigwa na yeye imekuwa moja ya kitu ni angalawe umkwide kama unataka kumtoa roho kimaumivu ndio anaona leo shughuli tamu!:-(

Mwisho NAKIRI nakubaliana na karibu yote ULIYOSEMA ila tu ,...
... tukumbuke kama kitu kina muhusu BINADAMU ,...
.... ni muhimu kujaribu kuepuka KUJENERALAIZI mambo kwa kuwa kuna watu MAUMIVU ni aina ya UTAMU na akienda hata GYM kufanya mazoezi kabla misuli haijauma hajisikii vizuri!

Nimewaza tu kwa SAUTI!:-(

Susan Wamunza alisema ...

Ni kweli Simon ulivyosema ila kwa Dunia ya sasa hauwezi kuepuka maumivu ya mapenzi mana imekuwa kama fashion.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom