Pamoja na kwamba upendo wa kweli huonekana machoni , kumbuka ili kumjua mwenza anayekupenda ni vitendo vyake anavyovifanya na si kwa kulazimishwa, ila ni kutokana na upendo alionao juu yako huo ndiyo upendo asili, na hii ipo tofauti sana na mwenza anayejfanyisha au kujilazimisha na ili kumjua mwenza wa namna hiyo utaona tu matendo yake mfano kama kweli anakujali na mliahidiana kuonana akachelewa,,au kuzima simu bila sababu,, kama ikitokea hali kama hii kwa mwenza anayemjali mpenzi wake lazima atakuwa makini sana na ahadi, na pia mwenza anayekupenda kwa dhati hupenda kuwasiliana na wewe mara kwa mara katika kukujulia hali au wakati mingine kupenda kuwa karibu na wewe huku akikutamkia maneno ya upendo. |
Maoni 3 :
Ni kweli mpendwa, pendo la asili, ni lile mnapotupiana jicho kwa mara ya kwanza, paah, moyo lipu....mmh, swali linakuja je linadumu!
Kudumu au kutodumu kwa pendo, ni nyie wenyewe wapendwa, kuwekana karibu, kujuana na jinsi gani ya kulicheza sebene, mawazo na kujaliana..nk hilo lipo wazi, au?
Adella,mahusiano yana mambo mengi sana ambayo ukiyatafsiri vibaya yatakuumiza. Kuna kaka mmoja ambaye ana mahusiano ya nje na yale ya girl friend wake, huyo girlfriend ni mcharuko, yaani matusi na ngumi mkononi....... Sasa kila saa anamtumia meseji "WAPI?", icheki vizuri hiyo msg sio uko wapi sweetie ila wapi? Nia ajue yuko wapi ili yeye akapumzike sehemu nyingine tofauti na aliyopo huyo girlfriend wake. Kwahiyo, sio kila saa unapotumiwa msg na mpenzi uko wapi honey, umekula? na vitu kama hivyo ni kwamba anakujali sana NO, ingawaje wengine humaanisha msg zao.
Pia kuna wengine hukupeleka na gari kokote unakotaka kwenda, na atakwambia ntakufuata, nia ni kufanya atakachokukifanya akijua hutamkuta.
Umakini unatakiwa sana katika mahusiano.
Pendo linaweza kutafsiriwa kwa maana mbalimbali, kama vile upendo, mapendo, mapenzi n.k.
Hapa linatumika kwa maana ya ono mojawapo la msingi kwa binadamu na wanyama ambalo wanavutiwa na jambo fulani, hata likafuatwa na hamu na hatimaye furaha ikiwa jambo limepatikana kweli.
Kati ya haja za msingi za nafsi, mojawapo ni kupenda na kupendwa.
Chapisha Maoni