Jumatatu, Mei 09, 2011

Upendo wa asili na wa dhati daima huonekana machoni

Pamoja na kwamba upendo wa kweli huonekana machoni , kumbuka ili kumjua mwenza anayekupenda ni vitendo vyake anavyovifanya na si kwa kulazimishwa, ila ni kutokana na upendo alionao juu yako huo ndiyo upendo asili, na hii ipo tofauti sana na mwenza anayejfanyisha au kujilazimisha na ili kumjua mwenza wa namna hiyo  utaona tu matendo yake  mfano kama kweli anakujali na mliahidiana kuonana akachelewa,,au kuzima simu bila sababu,, kama ikitokea hali kama hii kwa mwenza anayemjali mpenzi wake lazima atakuwa makini sana na ahadi, na pia mwenza anayekupenda kwa dhati hupenda kuwasiliana na wewe mara kwa mara katika kukujulia hali au wakati mingine kupenda kuwa karibu na wewe huku akikutamkia maneno ya upendo.
Pia kumbuka upendo wa kweli na wa asili hujionyesha pale mwenza wako  atakapo kuwa tayari kukutetea kwa jambo lolote , kuongozana na wewe na hata kukutambulisha kwa rafiki , ndugu na jamaa zake bila ya kukuonea aibu kwani wapo baadhi ya watu hushindwa hata kutoka na mwenza wake au kumtetea katika jambo ambalo anaona kabisa mpenzi wake anaonewa huyo utakuta hana mapenzi ya kweli.

Epuka mwenza anayependa mahusiano ya siri, ambaye siku zote humuwia vigumu kukutambulisha kwa rafiki zake au ndugu zake lakini katika hili pia yupo yule ambaye yeye ndiye hataki kutambulishwa unakuta mwenzake anapenda kumtambulisha lakini yeye anakataa ni lazima atoe sababu kwa nini hataki vinginevyo hana upendo wa kweli

Kingine ni kwamba siku zote ukitaka kufanikiwa kumuonyesha mpenzi wako namna unavyompenda ni lazima uwe na upendo wa asili na si wa kulazimishwa jaribu kuwa makini na ahadi zako katika mambo mbalimbali, heshima, na upendo wa dhati ni muhimu kuuzingatia ili usimpoteze yule unayempenda na hii ni kwa wote haijalishi ni mwanamume au mwanamke.

Maoni 3 :

emu-three alisema ...

Ni kweli mpendwa, pendo la asili, ni lile mnapotupiana jicho kwa mara ya kwanza, paah, moyo lipu....mmh, swali linakuja je linadumu!
Kudumu au kutodumu kwa pendo, ni nyie wenyewe wapendwa, kuwekana karibu, kujuana na jinsi gani ya kulicheza sebene, mawazo na kujaliana..nk hilo lipo wazi, au?

Bila jina alisema ...

Adella,mahusiano yana mambo mengi sana ambayo ukiyatafsiri vibaya yatakuumiza. Kuna kaka mmoja ambaye ana mahusiano ya nje na yale ya girl friend wake, huyo girlfriend ni mcharuko, yaani matusi na ngumi mkononi....... Sasa kila saa anamtumia meseji "WAPI?", icheki vizuri hiyo msg sio uko wapi sweetie ila wapi? Nia ajue yuko wapi ili yeye akapumzike sehemu nyingine tofauti na aliyopo huyo girlfriend wake. Kwahiyo, sio kila saa unapotumiwa msg na mpenzi uko wapi honey, umekula? na vitu kama hivyo ni kwamba anakujali sana NO, ingawaje wengine humaanisha msg zao.
Pia kuna wengine hukupeleka na gari kokote unakotaka kwenda, na atakwambia ntakufuata, nia ni kufanya atakachokukifanya akijua hutamkuta.
Umakini unatakiwa sana katika mahusiano.

Unknown alisema ...

Pendo linaweza kutafsiriwa kwa maana mbalimbali, kama vile upendo, mapendo, mapenzi n.k.

Hapa linatumika kwa maana ya ono mojawapo la msingi kwa binadamu na wanyama ambalo wanavutiwa na jambo fulani, hata likafuatwa na hamu na hatimaye furaha ikiwa jambo limepatikana kweli.

Kati ya haja za msingi za nafsi, mojawapo ni kupenda na kupendwa.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom