Ijumaa, Agosti 19, 2011

"mpenzi wangu ananipenda lakini nakerwa na tabia yake ya kunipiga"

Mimi ni mwanamke nipo katika uhusiano takribani miaka sita nampenda sana mpenzi wangu na tunamalengo mengi ya baadaye tatizo ni kwamba mpenzi wangu tabia yake ya hivi karibuni inanikera sana amekuwa akinipiga mara kwa mara kiasi kwamba mwili wangu umepata makovu lakini baada ya kunipiga huwa anajirudi na kuniomba msamaha mimi inaniuma sana nimeshajaribu kumrekebisha inashindikana.

Na mara nyingi hunipiga kwa makosa ambayo hata sielewi mfano anaweza kuchukua simu yangu akikuta jina la mwanamume anaanza kuwa mkali na kunipiga bila hata ya kufahamu ukweli hivi majuzi alinipiga baada ya kunikuta naongea na kijana mmoja wa mtaani kwetu sasa hivi nimemuambia bora tuachane analia huku akisema ananipenda yaani nimechoka jamani

Maoni 7 :

Bila jina alisema ...

Pole sana kwa masahibu hayo. Lakini ningependa kukupa ushauri mdogo tu. Kama mpenzi wako hataki uongee na hao vijana wa mtaani, we unaongea nao wa nini? Kama hataki kuona jina la mwanamme kwenye simu yako we unahifadhi majina hayo kwa nini? Kama unampenda msikilize. Na kama sijakosea umesema tabia hiyo ameanza hivi karibuni, kuna uwezekano mkubwa ameona mienendo yako imebadilika! Inabidi urudi nyuma na kuangalia wapi unakosea urekebishe ili kukabialiana na hili.

Bila jina alisema ...

Mwenzangu Mimi nakushauri achana Naye atakuja kukuua buree

Bila jina alisema ...

Ni wewe unampenda lakini yeye hakupendi. Mtu anayekupenda hata kupia hata siku moja...

Hii tabia ya kizamani mpaka leo mnazipalilia na kusema ati ananipenda lakini ananipiga..

Wewe ndio una future goals naye lakini yeye hana na wewe kabisa.

Kwanza read men don't hit women.

Bila jina alisema ...

YANI WEWE DADA UNAONEKANA UNA AKILI YA KITOTO SANA SINA UHAKIKA KAMA MZIMA BUT AM NOT SURE

Bila jina alisema ...

dada unajidanganya mwanauma anaekupenda hakugusi hata ! wewe unampenda yeye hakupendi hata kidogo ! pole bado hujui mwanamke anapendwaje mwanaume anaekupenda hataki kuona una maumivu yoyote huyo anaekupiga Ha!!!!! mi naona unapenda kupigwa usituambie anakupenda anataka uondoke na wewe hujielewi kaa hapo upigwe ukipata kilema ndo utajua unapendwa au LA !!!!!!! ya kizamani hayo sasa hivi tumeelimika na wao pia wameelimika

Bila jina alisema ...

Miaka sita na kupigwa juu bado una imani na mwanaume huyooooooo?? Miaka sita mnangoja nini na mnafanya nini?

Miaka sita umeambulia kupigwa na kuongezewa makovu badala ya kuongezewa love na watoto.Na wewe umeridhika kihivyo?Nina mashaka na wewe inaelekea hujiamini na labda hupendeki ndiyo maana anakudunda na wewe bado unang'ang'ana hapohapo.

Bila jina alisema ...

sasa unampendea nini kama anakupiga? Kwani wewe ni ngoma? Hivi upendo mnauelewaje ninyi?

Unajeruhiwa bado unasema eti unampenda mtu heeeeeeeeeeeeee!! Hiyo kali haswa??????

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom