Jumanne, Agosti 30, 2011

"Mume wangu aniamini anasema mtoto niliyemzaa siyo wake"

Habari yako Adela pole na majukumu mimi ni mwanamke nimeolewa tumeishi na mume wangu takribani miaka mitatu nampenda sana mume wangu lakini kwa hili lililotokea amenishangaza sana mimi nilichelewa kupata ujauzito lakini baadaye Mungu alinisaidia nikabeba ujauzito ambapo mume wangu alifurahi sana.

Lakini baada ya kujifungua amemkana mtoto na kusema si wa kwake tena akishirikiana na mama yake mzazi huku akisema kwao wote kuna alama wanazaliwa nayo na mtoto niliyemzaa mimi hiyo alama hana ameshanitukana sana na kuniambia kuwa nimemsingizia ujauzito ukweli kabisa mimi sijawahi kumsaliti mume wangu na cha ajabu nimemuambia tukaangalie katika vipimo vya DNA ananijibu haina haja kwani ukweli umeshaonekana inaniuma sana jamani naombeni ushauri wenu.

Maoni 4 :

Bila jina alisema ...

pumbavuuuuuuuuuu. Huyo mwanamme akili zake fupi, mpungufu kabisa. Na mama yake ni mwanga.

Mie ningemuambia kama aniamini basi bora tuachane maana watoto wote nitakao mzalia kama hawajazaliwa na alama hizo atawakataa.

Mulize huyu mtoto baba yake nani?

Alafu contakt Dina Marios, na mueleze hili swala, na omba ushauri kwa watalaam ili wamueleweze hilo dume jinga, katoka kijiji cha wapi huyo? yaonesha hata darasani hakuenda kama mama yake

Bila jina alisema ...

khaaa huyo mwanamume hana akili jamani basi analake jambo na huyo mama yake inaonekana hawakutaki nakushauri endelea kumsisitiza kuhusu DNA

Bila jina alisema ...

Huyo anajielewa udhaifu wake ndio maana anakusingizia.Kwa kweli una mtihani mgumu kama ndio dizaini ya mume uliye naye???

Pole mwaya mpeleke kwa mchungaji wenu aliyewafungisha ndoa mkashauriwe na ikishindikana iteni wazazi wenu wote wa pande mbili awaeleze kilichojiri.kwani lazima wao ndio wamlande mtoto?je kama anafanana na wa ukoo wa mwanamke?'

Huyo mpuuuuuuuuzi kabisa.Tena ametuaibisha sisi wanaume.

Rik Kilasi alisema ...

Daah inaumaje? kama hataki amini kwanini msipime DNA au kapata mwingine anatfuta sababu? lkn upande wa pili wa shilingi huwezi jua penginehuyo mumeo anajijua hana uwezo wa kuzalisha baada ya kuruka ruka huku na kule peku peku ila DNA ndio jibu kwasasa kuimarisha ndoa yako otherwise utaambiwa huyo umemtafuta nje ya ndoa kama anavyodai kwa sababu zake binafsi au kushawishika na ndugu eti alama! nini alama bana duh!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom