Jumapili, Septemba 04, 2011

"mimi ni mwanamume natafuta mchumba wa ukweli "

Msaada dada Adela!
Kwanza hongera kwa kazi yako nzuri.
Ni hivi,
Natarajia kurudi nyumbani Tz hivi karibuni baada ya mihangaiko ya hapa na pale huku Ughaibuni. Kwa umri nilionao hivi sasa (37) nahitaji kuwa na familia. Ningependa kupata mwenza (mke) hapo kwetu nyumbani ili Mungu akijalia tulifanikishe hilo. Mke wangu mtarajiwa ningependa awe na umri kati miaka 25 mpaka 35,  elimu kidato cha nne na kuendelea, awe tayari kuishi maisha ya ndoa na kujenga familia imara. Kwa aliye tayari aniandikie kupitia email ifuatayo:  ngulafarahani@yahoo.com
Asante.

Maoni 10 :

Bila jina alisema ...

HI ADELA, HOPE YOU DOING WELL, mie ninaona huyu kaka au hao wanaotafuta wachumba waweke na picha zao ,ndo wanaweza kujipatia wanaowatafuta kwa kirahisi...lol..anyway hayo ni maoni yangu tu. keep up the good work dear..

Bila jina alisema ...

Aende hapa: www.wabongomeet.com ajichagulie mchumba anayetaka.

Bila jina alisema ...

Aende tu Wabongomeet.com, wachumba wengi wapo. Pia kuna wadada wengi wamejaribu kutuma email haiendi atakuwa hamaanishi maana email yake si ya kweli.

Bila jina alisema ...

Amuandikie dada mmoja tunafanya naye kazi anaitwa jack.mushil@gmail.com kwa kweli ni mwanamke mwema na hautajutia maisha yako yote

Farahani alisema ...

Nawasukuru wote kwa michango yenu. Kimsingi niko serious sana katika hili. Namshukuru pia mchangiaji alitoa taarifa juu ya kugoma kwa email. Kuna kosa la kiuandishi limefanyika. Naomba radhi kwa hilo. Email yangu sahihi ni: farahaningula@yahoo.com

Bila jina alisema ...

uyo kaka anayetafuta mchumba .. atoe namba yake ya sim coz email yake haitambuliki ..

Bila jina alisema ...

wabongo meet ni fake.Mimi nimejaribu sana kuwaandikia hao mademu lakini hakuna aliyejibu kwa muda mrefu.Nafikiri huyo bloger amebuni tu majina na kuandika profile ili watu wamwagike kutembelea blog yake maana ni ngeni.Uswahili mtupu kabisaaaaaaa.

Bila jina alisema ...

Mchangiaji hapo juu anasema huyo email ya huyo kaka haifanyi kazi. Lakini naona kama kaka mwenyewe amerekebisha kwa kuweka email yake sahii baada ya kukiri kuwa ya kwanza ilikuwa na makosa. Soma kwa mchangiaji wa tano kutoka juu.

Bila jina alisema ...

Hi,
Kaka naamini mpaka umeamua kutoa ombi lako kwenye blog hii maana yake una shida, na pia watakaokuandikia pia wana shida kwenye jambo hili. Hivyo kama uko serious jaribu kutoa majibu mazuri kwa wote watakaokuandikia.Sio kuwaona kama wanashiiiiiida unless haujua maana ya kutoa shida yako kwenye blog hii. I wish u all the best.

Bila jina alisema ...

Kaka furaha mke mwema anatoka kwa Bwana, wanawake wapo wengi na wakila aina ila mke anatoka kwa Bwana.
So muombe yeye naye atakupa wa kwako ambaye atakuwa sawasawa na haja yako maana yeye anakujua na anajua ni yupi anakufaa kuwa wa kwako. Ukiwa na haraka katika hili au ukaangalia kwa jinsi unayotaka ndio yale ya kupata mke wa kichina ambaye baada ya muda kuingia ndani ya ndoa wakuta ni feki. Mimi nimeona raha ya kuomba maana nimepata mume mwema ambaye tunafanana katika mambo mengi ikiwemo kimawazo, mipango na hata mambo ya mapenzy tunafurahiana sana maana wote tupo huru.
Kama lilivyo jina lako furaha basi omba Mungu ili yeye akupe furaha.
Cathy

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom