Jumatatu, Septemba 19, 2011

Rafiki yangu ananikera na tabia yake ya kumsifia mke wangu kila anapomuona,,,

Mimi ni mwanamume nina mke na watoto wawili nampenda sana mke wangu tumeishi takribani  miaka saba, tatizo linakuja ninaye rafiki ambaye ni rafiki yangu wa miaka mingi sikuhizi ananishangaza na tabia yake ya kumsifia mke wangu mara kwa mara akimuona anamwambia wewe ni mwanamke mrembo sana ningekuwahi ningekuoa mara anamsifia anapendeza sana akivaa vimini na magauni ya kubana akimkuta ametoka saluni atamsifia kama dakika ishirini mimi huwa nanyamaza kimya sasa hivi majuzi alinikera zaidi nilimkuta nyumbani kwangu akinisubiri huku amemletea mke wangu zawadi ya gauni eti anasema aliliona akajua litampendeza sana shemeji yake mimi inanishangaza sana je huyu rafiki yangu si anaweza kuwa anamtaka mke wangu naombeni ushauri marafiki kupitia blog ya Adela.

Maoni 11 :

Yasinta Ngonyani alisema ...

Inawezekana anampenda na inawezekana anampenda kama shemeji yake..labda cha muhimu ni kumuuliza kama anampenda kivipi?

Bila jina alisema ...

hapo ni ushauri ngani unaouomba? mbona jibu unalo? kifupi ndio hivyo nikiasi cha kumkanya mbele ya mkeo na yeye mwemywe akiwepo na pia mpige marufuku kuja home wakati wewe haupo...........
Rida

Mama Melvin alisema ...

duh! huyo si rafiki mzuri uwe makini nae. mulika mwizi.

emuthree alisema ...

Cha muhimu ni wewe na mkeo muwe kitu kimoja. Mimi nina imani kuwa mtoto akishiba vyema hawezi kwenda kudoea kwa jirani!Cha muhimu ni wewe na mkeo muwe kitu kimoja. Mimi nina imani kuwa mtoto akishiba vyema hawezi kwenda kudoea kwa jirani!

Bila jina alisema ...

Keshakula huyoo...Wewe eti unaomba ushauri hapa wakati mwenzio anapakua vilivyo vyako !!!

Bila jina alisema ...

hahahahahahaaaaa !! Utaipata ndugu.Huyo kishaanza kummezea mkeo.Hizo zawadi ni utongozaji.Na ukute wewe humnunulii chpochote haraka sana atahamishia upendo kwa huyo jamaa,si unajua wanawake walivyo dhaifu waweza kudanganywa na kitu kidogo kwani wanapenda sana kusifiwa kwa kila jambo na vaaji.Huyo rafiki yako amempatia sana mkeo.kama wewe humsifii basi ujue inakula kwako.Poteza kabisa urafiki na mtu wa namna hiyo.kwa sababu ni rafiki yako wa muda mrefu hebu mkanye mkeo kuwa amwambie kuwa anavyomfanyia hapendezwi kabisa mbele ya mumewe.Si ajabu hata kutomba kisha mega jamaa,hiyo kali utaliwa usipoangalia.

Simon Kitururu alisema ...

Kwani unamuogopa?
Mwambie na mwambie mkeo kuwa huhusudu hicho kitu!

Ukiachia anaweza kuneemeka kwakuwa hata mkewe au hata yeyey mazingira yakijipa wanaweza halalaisha wakijua kuwa mbona mwenyewe ukouko tu !


Ni moja tu ya mtazamo na mitazamo katika hili huweza kuwa milioni!:-(

Bila jina alisema ...

haha!! mulika mwiziii...

Bila jina alisema ...

Jamaa amekudharau sana! Haya mambo ya namna hiyo hayawezi kutokea MUSOMA!!!

Bila jina alisema ...

Pengine kaona unamnyanyasa mkeo. Au unacheat sana. Au kaona haumtunzi vizuri mkeo. Au kaona unamdharau mkeo. Na anakufundisha jinsi ya kutunza mke.

labda kaona wewe unamkosoa mkeo, haumsifi.

Hakika kama angekuwa anamtaka kimapenzi hasingefanya hivo mbele yako.

Labda huyo rafiki yako awe muuni sana, au mlevi sana.

Bila jina alisema ...

baba fanya wajibu wako tu hakuna kubabaika. naungana na aliyesema mtoto akishiba hawezi kudoea vya nyumba ya jirani. Kama wewe unamfanyia mema ikiwemo hilo la kumsifia hatababaika na kusifiwa na mwingine. Hofu nyingi kwenye mahusiano hasa ya kimapenzi zinakuwepo kama mtu hafanyi wajibu wake matokeo yake kelele zinakuwa nyingi. Simama kwenye nafasi yako

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom