Jumapili, Desemba 04, 2011

Raha ya mwanamke kujipamba na kwenda na wakati.

Mwanamke anatakiwa kuwa pambo mwenye kujinakshi na kuvutia, na kumbuka kwamba uzuri wa mwanamke huongezeka zaidi pale ambapo atajipamba na kujinakshi. Kwanza kabisa mwanamke anatakiwa haijali ngozi yake kwa kutumia vipodozi vinavyoendana na ngozi yake na vipodozi hivyo ni vyema vikawa vya asili ambavyo vimetengenezwa viwandani

zingatia mapambo ya mwili kama mikufu, hereni saa ya mkononi, bangili , pete na kadhalika na pia itapendeza ukiwa nazo tofauti tofauti  ili ikusaidie katika kujinakshi na nguo zako. Pia hakikisha kabati lako ama begi lako la nguo lina nguo muhimu za kazini, nyumbani, na za kutokea na hii itakupa urahisi wa kupangilia mavazi yako pindi upatapo safari ya dharura kwa kuzingatia haya unaweza tembelea blog ya mwanadada mrembo pichani http://www.8020fashion.blogspot.com  utapata kuona mitindo ya aina mbalimbali na watu wanavyopendeza kwa kujipangilia mavazi kulingana na sehemu husika
mwanamke unatakiwa kuwa na poda inayoendana na ngozi yako, wanja, lipstic au lipbam uipendayo sambamba na pafyumu, usisahau kuwa na bidhaa za nywele kama vile mafuta, spray pink losheni nakadhalika

Halafu malizia na viatu angalia viatu vizuri vinavyokwenda na wakati na vyenye kukufaa na kukuweka huru utembeapo Mwanamke ni kujipamba na kwa kufanya hivyo utafurahia maisha popote huendako kwa kujiweka nadhifu wakati wote.

Maoni 4 :

Bila jina alisema ...

Adela asante kwa ushauri kipenzi

Bila jina alisema ...

jamani wewe unangozi nzuri unatumia nini nipe siri mwenzio naitwa Sara

Bila jina alisema ...

pamoja sana mamito ushauri mzuri mwanamke kujipamba mwenzagu

Bila jina alisema ...

pamoja sana mamito ushauri mzuri mwanamke kujipamba mwenzagu

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom