Ndani ya kitabu hiki nimezungumzia maisha na mapenzi katika mtazamo halisi na pia kinaonyesha namna mapenzi yanavyoweza kuyageuza maisha kuwa machungu na mafupi. |
Ukianza kusoma kitabu hiki hutakiacha hadi ukimalize kwani hadithi zilizomo zimesheheni matukio ya kusisimua ambayo moja kwa moja yanalenga maisha yetu ya kila siku. |
Kupitia vitabu vya simulizi za maisha kama vile kitabu hiki, tunajifunza mambo mengi ambayo yanatusaidia kuishi katika mazingira tofauti ikiwa ni katika shida au raha na hata kujua namna ya kuishi na watu wanaotuzunguka.
Utapata kitabu hiki kwa bei ya sh 5000 tu.
Kwa mawasiliano kuhusu upatikanaji wa kitabu hiki.
Tafadhali tumia no zifuatazo +255652343430 au +255752817444
Au niandikie kupitia kavisheadela@yahoo.com
Natarajia pia kufanya uzinduzi wa kitabu Mungu akinijalia nitafurahi kuwaalika pia wadau wangu katika uzinduzi.
Maoni 12 :
waooooooooo mdada kitabu ntakitafuta maana hadithi tamu na kwenye uzinduzi usinikose hongera mwaya wanawake tunaweza
Asante sana Lulu tuko pamoja usijali tuwasiliane utapata kadi ya mwaliko tuko pamoja sana
Hongera sana mpendwa, umenipa faraja fulani, kumbe inawezekana kutunga na kucha kitabu, nitakutafuta....
hongera sana Adela! kwa kweli hiyo ni hatua ya kuigwa, umekua mbunifu mzuri sana pia ktk kuendeleza fasihi andishi ambayo naona kama kwa sk za karibuni waandishi wengi wamejikita ktk kuandika hadithi magazetini zaid kuliko kutoa vitabuni, japo ndio ni gharama lkn penye nia pana njia!
Hongera tena na Mungu akutangulie ktk Maono yako Adela
Hongera sana Adela nitakitafuta kitabu
Uko juu mdada utafika mbali sana
hongera adella unakipaji unaweza ht ukawa unawatungia story za movie dah! uko juu
yaani nakuhitaji hicho kitabu sana kwasababu nakubali sana kazi yako huwa nakusikiliza kupitia radio passion fm una kipaji cha utunzi na kuelimisha jamii
Adela jamani kitabu nitakipataje napenda sana simulizi my dear
Adela mimi sina wasi wasi na hiki Kitabu, ntakipata tu kikiingia mtaani, ntakutafuta. Upo juu zaidi ya Mawingu Adela!!
Hongera sana..Kiweke basi kwa ebook tununue wengi hata tusio nyumbani sasa hivi..
Check hii site https://www.payloadz.com/
Hi samahani sis, nikitaka kununua kitabu chako sijui nitakipataje na ni bei gani? Me niko UK my email is geraldelton@yahoo.co.uk.
Thanx
Chapisha Maoni