Ijumaa, Machi 09, 2012

MALIPO NI HAPA HAPA,,, MALIPO NI HAPAHAPA.,,,,MALIPO NI HAPAHAPA

  JINA LA KITABU      MALIPO NI HAPAHAPA
      MTUNZI                  ADELA DALLY KAVISHE
Ninayofuraha kukamilisha kitabu cha simulizi cha MALIPO NI HAPAHAPA ambacho kimebeba simulizi tatu za kusisimua ikiwemo simulizi inayoitwa DADA YANGU ambayo naendelea kuiweka katika blog lakini pia kuna simulizi inaitwa MAMA MDOGO pamoja na simulizi iliyobeba jina la kitabu MALIPO NI HAPAHAPA

 
Kitabu cha Malipo ni Hapahapa na simulizi nyingine za maisha kinaonyesha hali halisi ya maisha tunayoishi, matatizo tunayokutana nayo na namna ya kutatua matatizo tunayoyapata kwa wakati huo. Pia kwa kusoma kitabu hiki utajifunza mengi kwani kinatoa  picha halisi ya maisha yetu ya kila siku.


Ndani ya kitabu hiki nimezungumzia maisha na mapenzi katika mtazamo halisi na pia kinaonyesha namna mapenzi yanavyoweza kuyageuza maisha kuwa machungu na mafupi.

Ukianza kusoma kitabu hiki hutakiacha hadi ukimalize kwani hadithi zilizomo zimesheheni matukio ya kusisimua ambayo moja kwa moja yanalenga maisha yetu ya kila siku.

Utajifunza mambo mengi sana kupitia kitabu hiki ni matumaini yangu tutakuwa pamoja wadau ushirikiano wako ni wa muhimu sana kwangu natarajia kitabu cha MALIPO NI HAPAHAPA kitapatikana mtaani hivi karibuni.


Kupitia vitabu vya simulizi za maisha kama vile kitabu hiki, tunajifunza mambo mengi ambayo yanatusaidia kuishi katika mazingira tofauti ikiwa ni katika shida au raha na hata kujua namna ya kuishi na watu wanaotuzunguka.

Utapata kitabu hiki kwa  bei ya sh 5000 tu.
 Kwa mawasiliano kuhusu upatikanaji wa kitabu hiki.
Tafadhali tumia no zifuatazo +255652343430 au +255752817444
Au niandikie kupitia kavisheadela@yahoo.com

 Natarajia pia kufanya uzinduzi wa kitabu Mungu akinijalia nitafurahi kuwaalika pia wadau wangu katika uzinduzi.


Maoni 12 :

lulu ibrahim alisema ...

waooooooooo mdada kitabu ntakitafuta maana hadithi tamu na kwenye uzinduzi usinikose hongera mwaya wanawake tunaweza

ADELA KAVISHE alisema ...

Asante sana Lulu tuko pamoja usijali tuwasiliane utapata kadi ya mwaliko tuko pamoja sana

emu-three alisema ...

Hongera sana mpendwa, umenipa faraja fulani, kumbe inawezekana kutunga na kucha kitabu, nitakutafuta....

Bila jina alisema ...

hongera sana Adela! kwa kweli hiyo ni hatua ya kuigwa, umekua mbunifu mzuri sana pia ktk kuendeleza fasihi andishi ambayo naona kama kwa sk za karibuni waandishi wengi wamejikita ktk kuandika hadithi magazetini zaid kuliko kutoa vitabuni, japo ndio ni gharama lkn penye nia pana njia!

Hongera tena na Mungu akutangulie ktk Maono yako Adela

Bila jina alisema ...

Hongera sana Adela nitakitafuta kitabu

Bila jina alisema ...

Uko juu mdada utafika mbali sana

Bila jina alisema ...

hongera adella unakipaji unaweza ht ukawa unawatungia story za movie dah! uko juu

Bila jina alisema ...

yaani nakuhitaji hicho kitabu sana kwasababu nakubali sana kazi yako huwa nakusikiliza kupitia radio passion fm una kipaji cha utunzi na kuelimisha jamii

Bila jina alisema ...

Adela jamani kitabu nitakipataje napenda sana simulizi my dear

Unknown alisema ...

Adela mimi sina wasi wasi na hiki Kitabu, ntakipata tu kikiingia mtaani, ntakutafuta. Upo juu zaidi ya Mawingu Adela!!

swahilimom alisema ...

Hongera sana..Kiweke basi kwa ebook tununue wengi hata tusio nyumbani sasa hivi..

Check hii site https://www.payloadz.com/

Bila jina alisema ...

Hi samahani sis, nikitaka kununua kitabu chako sijui nitakipataje na ni bei gani? Me niko UK my email is geraldelton@yahoo.co.uk.
Thanx

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom