Katika maisha kuna baadhi ya watu hususani wanawake kuwa na tabia ya kufurahia mwanamke mwenzake anapoachika, kwa mfano labda alikuwa ameolewa akisikia tu kwamba ameachika au katika ndoa ya huyo rafiki yake kuna migogoro basi kwake ni sherehe jamani sote ni binadamu kuna leo na kesho inapotokea mwenzio ana matatizo katika uhusiano alionao kwako isiwe furaha "Eti ooh yamemkuta ndiyo akome sasa alikuwa anajishebedua na huyo bwanaake sasa ameachika tuone ataishi vipi mjini" Haya ni baadhi ya maneno utawasikia wanaofurahia uhusiano wa fulani kuvunjika. |
Maoni 2 :
Kweli kabisa! Nimeifurahia sana article yako. Mie nashindwa kuelewa saa nyingine kwanini hatupendani hivi? wanawake tunahitaji umoja.
peleka ujina huko unafikiri mtu atashabikia bila kuwa nasababu
Chapisha Maoni