Jumapili, Aprili 01, 2012

Si vyema kufurahia inapotokea mwenzako ameachika ama kuachwa na mwenza wake

Katika maisha kuna baadhi ya watu hususani wanawake kuwa na tabia ya kufurahia mwanamke mwenzake anapoachika,  kwa mfano labda alikuwa ameolewa akisikia tu kwamba ameachika au  katika ndoa ya huyo rafiki yake kuna migogoro basi kwake ni sherehe jamani sote ni binadamu kuna leo na kesho inapotokea mwenzio ana matatizo katika uhusiano alionao kwako isiwe furaha "Eti ooh yamemkuta ndiyo akome sasa alikuwa anajishebedua na huyo bwanaake sasa ameachika tuone ataishi vipi mjini" Haya ni baadhi ya maneno utawasikia wanaofurahia uhusiano wa fulani kuvunjika.
Halafu watu hao wakiona wawili wamependana yaani wapo na furaha katika mapenzi yao hawakosi la kusema "Tutaona wataishia wapi yaani wanajidai wanapendana" na mwingine anasema "Mapenzi yatakuwa bongo bwana wanadanganyana tu kwanza siku hizi hakuna mapenzi" Jamani chuki za nini? na kama mwenzio akiachika au kaachwa wewe unafaidika nini? kiukweli hii tabia ipo na si tabia nzuri MAPENZI HUWA HAYATABIRIKI LEO UTAFURAHIA MWENZIO KAACHWA KESHO KWAKO IKITOKEA JE UTAFURAHI HIVYOHIVYO.....................

Maoni 2 :

Bila jina alisema ...

Kweli kabisa! Nimeifurahia sana article yako. Mie nashindwa kuelewa saa nyingine kwanini hatupendani hivi? wanawake tunahitaji umoja.

Bila jina alisema ...

peleka ujina huko unafikiri mtu atashabikia bila kuwa nasababu

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom