Habari Adela mimi ni mdau wa Blog yako na hongera sana kwa kuelimisha jamii kupitia simulizi zako nzuri mimi nina tatizo naomba uniwekee kwenye blog yako nipate ushauri, Nina mke na watoto wawili familia yangu ninaipenda sana lakini tatizo ni mke wangu yaani nikichelewa kurudi nyumbani ikiwa ni katika kazi zangu za kila siku au matatizo yoyote yanayotuhusu sisi wawili anaenda kuwaambia marafiki zangu huku akisema mimi sijatulia, na niliwahi kumkalisha chini na kumuambia sipendi anavyoenda kuwaambia maneno marafiki zangu ni bora anieleze mimi mwenyewe lakini naona tabia hiyo bado inaendelea hivi majuzi ndiyo nilikereka zaidi rafiki yangu alikuja akaniambia kuwa jitahidi umridhishe mke wako mnamo sita kwa sita analalamika sana,,, niliumia sana moyoni na kujiuliza huyu mwanamke hadi mambo ya chumbani anatoa nje yaani nikipita mtaani marafiki zake wananijua kila kitu na marafiki zangu hivyohivyo hii tabia imenichosha wakati mwingine najuta kwanini nilimuoa
Maoni 5 :
mmmmmh mwanamke gani mmbeya kiasi hicho jamani duuuh inabidi uzungumze naye tena jaribu hata kumtishia kuwa utamuacha kama anaendelea na tabia yake hiyo
duh iyo sasa kali mpka ya chumbani anatoa nje?mpe somo au kwao hajafundwa vzr???? mna mtu kma unahakili uwezi toa siri zako za chumbani!pole sana kaka angu,mda mwingne wanawake ndio coz ya kufanya waume zao watafute nyumba ndgo.
Kama hujiwezi mambo ya bed room tukusaidie ndugu usije umbuka bure? Huyo mwanamke na mdomo wazi maana mambo kama hayo hayafai kabisa kuyatoa nje ya eneo lenu.Vumilia tu maana ulishayavulia nguo.Angekuwa wangu ningemtosa kabisaaaaaa
Jamani Adella nimeshangaa kweli huyo dada hajafundwa? maana mwanamke makini hawezi kutoa siri za mume wake nje, pole sana kaka kwa masaibu hayo
kaka uyo mkeo hana akili ata kidogo mkalishe chini umweleze kutokana na tabia yake na jinsi usivyopendezwa nayo ikiwezekane mpeleke ata kwatu wazima unaowaamini wamuelekeze asipoelewa kote uko achana nae ndoa sio mateso
Chapisha Maoni