ILIPOISHIA
Nilimshika mikono huku nikimbembeleza kwasababu alikuwa na hofu sana nilimchukua na kwenda naye sebuleni kisha nikamuuliza taratibu. Kilichonishangaza Renata alinisimulia ndoto aliyokuwa anaiota ilikuwa inafanana vilevile na ndoto ya kutisha niliyokuwa nikiota.Nikiwa na hofu kubwa na wasiwasi Charito alinitizama na kusema "Usiwe na wasiwasi mke wangu, haya ni majaribu ya shetani, kuwa na imani na Mungu kila kitu kitaenda sawa , usiogope chochote kwani shetani atashindwa kwa nguvu zake Mungu". JE NINI KITAENDELEA ....USIKOSE ....SURA YA ........27...
INAPOENDELEA
Nilikuwa
na wasiwasi na mawazo mengi sana kichwani,
na hata kujiuliza maswali mengi bila ya kupata majibu kwani sikuelewa ni
kwanini, maisha yangu yanaendelea kupata majaribu na wakati nimekwisha mpokea
Mungu katika maisha yangu. Siku zilienda huku nikiwa naota ndoto za ajabu kila
kukicha wakati mwingine nilikuwa nashindwa kulala kabisa, kutokana na hofu.
Siku
moja nilikuwa nimeketi sebuleni huku nikiwaza “Hivi inawezekana hii nyumba ya Mama Bilionea
imezindikwa na nguvu za giza ambazo haziwezi kuisha, na sasa mbona tunasali na
kukemea nguvu za giza kila siku kwanini
hali hii inajirudia, yaani mimi nimechoka na hii hali, haya ni mateso jamani ni
bora nimwambie mume wangu tuondoke katika hii nyumba vinginevyo na wasiwasi linaweza
kutokea tatizo”. Nilikuwa na mawazo mengi sana siku hiyo, nikiwa naendelea
kuwaza, Renata alikuja na kuketi karibu yangu huku akiwa amenyamaza kimya bila
ya kuzungumza chochote.
Nilimtizama Renata na kusema “Renata mbona upo kimya
sana, na tena unaonekana mnyonge vipi una matatizo mdogo wangu?” Renata
alinyama kimya kidogo na kisha akanijibu “Dada, hata nikikueleza matatizo
niliyonayo, wewe hauniamini, mimi usiku naona vitu vya ajabu, halafu kinachonishangaza
wakati mwingine namuona shemeji Charito akija chumbani kwangu usiku huku
akionekana kuwa katika umbo la ajabu na pia....” Kabla Renata hajamaliza
kuzungumza nilimkatisha na kusema
“Sikiliza nikuambie Renata, hizo ni ndoto tu na hazina maana mbaya, na
pia kumbuka kusali kabla ya kulala kwani hayo ni majaribu ya shetani, anaweza
kukufanya wewe umchukie shemeji yako”
Renata alinyanyuka kwa hasira pale alipokuwa amekaa na kusogea karibu yangu
“Nilijua tu, hauwezi kuniamini lakini dada kumbuka usilolijua ni sawasawa na
usiku wa kiza kinene, mimi naongea ukweli na wala siyo ndoto”.
Nilishangaa kumuona Renata katika hali ile, ikanibidi niwe mkali kidogo “Unajua Renata wewe ni mtoto mdogo sana kuzungumza na mimi kwa sauti kali kiasi hicho, mimi ni dada yako mkubwa na inabidi uniheshimu lakini sasa naona unapoelekea nitakuja kukupiga nikuumize vibaya, sijaipenda kabisa tabia yako, embu toka hapa sitaki kukuona nisije nikakunyofoa huo mdomo wako mchafu.” Renata aliondoka huku akisema “Sawa dada lakini ipo siku utaniamini”.
Nilishangaa kumuona Renata katika hali ile, ikanibidi niwe mkali kidogo “Unajua Renata wewe ni mtoto mdogo sana kuzungumza na mimi kwa sauti kali kiasi hicho, mimi ni dada yako mkubwa na inabidi uniheshimu lakini sasa naona unapoelekea nitakuja kukupiga nikuumize vibaya, sijaipenda kabisa tabia yako, embu toka hapa sitaki kukuona nisije nikakunyofoa huo mdomo wako mchafu.” Renata aliondoka huku akisema “Sawa dada lakini ipo siku utaniamini”.
Nilibaki
pale sebuleni huku nikizungumza na nafsi yangu “Sijui huyu mtoto amepatwa na
pepo gani jamani, yaani Renata ni wa kunipandishia sauti kana kwamba
tunalingana, mjinga sana.” Nilikuwa najisemesha peke yangu, baadaye niliingia
jikoni kuandaa chakula.
Baada ya
miezi miwili kupita, siku moja niliamka nikiwa najisikia nimechoka sana huku mwili wangu ukiwa na joto kali sana,
nilijihisi naumwa hivyo ilinibidi niende Hospitali kupima. Nikiwa nimeongozana
na mume wangu Charito tulifika hospitali
na Daktari alinitaka nipime haja ndogo pamoja na damu. Baada ya vipimo nilikaa
takribani robo saa na kwenda kuchukua majibu.
Vipimo
vilionyesha kuwa nilikuwa nina ujauzito. Nilifurahi sana huku nikimkumbatia
mume wangu kwa furaha “Charito, hatimaye sasa na mimi nitakuwa mama na wewe
utakuwa Baba, namshukuru sana Mungu leo
ni siku ya furaha sana” Charito alionyesha tabasamu usoni huku akisema
“Nimefurahi pia mke wangu, Mungu ni mwema”. Baadaye Daktari alinishauri, nipendelee
kunywa maji kwa wingi na kula mbogamboga na matunda.
Tulirudi
nyumbani tukiwa na furaha sana. Baada ya kuingia ndani nilimkuta Renata akiwa
ameketi chini ya mti uliokuwepo pale nyumbani, huku akilia na kutetemeka,
niliogopa sana kumuona katika ile hali na
haraka nilisogea karibu na kumuuliza ana matatizo gani “Umepatwa na kitu
gani Renata?” Renata alinijibu huku akiendelea kilia “Tumaini, Tumaini, Dada
Kandida Tumaini” Nilishindwa kumuelewa ikanibidi nimshike mikono “Tumaini
kafanya nini? Yuko wapi Tumaini” Nilihisi
kuna jambo baya litakuwa limepata mdogo wangu Tumaini. “Tumaini amepotea, alitoka nje akiwa anakimbia
na hajarudi tena, na mimi nilikuwa nilimfuata na kumtafuta bila mafanikio”
Nilinyamaza kimya kidogo na kutafakari “Inamaana Tumaini atakuwa ameenda wapi?
Na pia hajawahi kutoka akiwa peke yake hata siku moja, na kwanini amekimbia? Au
kuna mtu amemtorosha mdogo wangu”
Nilikuwa nawaza huku Renata
akinitikisa mkono kwa nguvu na kunivuta “Dada twende tukamtafute Tumaini,
twende dada” Wakati huo Charito alikuwa amesimama pembeni na kusema
“Inawezekanaje mlinzi alikuwepo hapa getini halafu mtoto anakimbia anashindwa
kumrudisha, sasa atakuwa amekimbilia wapi, si unajua Dar es salaam ni kubwa”
Alisema Charito huku akiwa anaelekea kumtafuta mlinzi na mimi nikawaza kuwa
hawezekani Tumaini akawa ameenda sehemu
ya mbali labda atakuwa maeneo ya karibu, haraka nilitoka nje na kuanza
kuwauliza majirani JE NINI KITAENDELEA USIKOSE...... SEHEMU YA........28.........
Maoni 5 :
Tatizo la kandida ni libishi sana kama moursin mbaraka wa misri, hataki kuckia wala kuambiwa na mdogo wake. atakiona kitakachofuatia.
Kadinda ananiuz ntamn nimnase vbao,htimae.linazaa jini,jitu gn bishi?????
Daaah! tokea awali kaambiwa na renata lkn kandida hataki kusikia la mdogo wake. akumbuke kuwa kuckia kwa kenge mpaka avuje damu sikioni.
Bora wahame kwenye hiyo nyumba ya huyo mama wakatafute nyumba nyingine, la sivyo wataanza kufa mmoja mmoja.
kadinda
Chapisha Maoni