Ijumaa, Mei 02, 2014

ALICHOKISEMA RAIS JAKAYA KIKWETE KWA WAFANYAKAZI SIKU YA MEI MOSI

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akimkabidhi hundi ya shilingi milioni 5, mfanyakazi bora wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Herman Kachima, wakati wan kilele cha siku ya Wafanyakazi Duniani ambapo kitaifa zilifanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar  es Salaam.
Rais Kikwete alisema anatambua kuwa wafanyakazi wana hamu ya kujua Serikali itasema nini kuhusu masilahi yao.Alisema malalamiko ya wafanyakazi wengi ni kutaka kuona kima cha chini cha mshahara kinaongezwa huku kodi kwenye mishahara (Paye), ikipungua.“Mimi na wenzangu serikalini hatuna upungufu wa dhamira ya kufanya hivyo, tumethibitisha miaka iliyopita na tutaendelea kuwa hivyo.
"Najua kuwa nyongeza tuliyotoa mwaka jana si kubwa kama wafanyakazi walivyotaka iwe... hata mimi nisingependa iwe hivyo.Kwa nyongeza iliyofanywa mwaka jana, hivi sasa Serikali inatumia asilimia 44.9 ya Bajeti kulipa mishahara ambayo ni asilimia 10 ya Pato la Taifa.”

Akifafanua namna Serikali ilivyofikia uamuzi wa kuongeza mishahara kwa mwaka huu, Rais Kikwete alisema kulikuwa na mjadala mkali baina ya wafadhili waliodai nyongeza ni kubwa mno.“Ni kweli mapato yetu ni madogo lakini kwa kuwa mishahara ni midogo, lazima tuendelee kuongeza, hata hicho kidogo lazima ukitoe ili uijenge ile nafuu, alisema bila kutaja kiwango kitakachoongozwa.
“Hata sasa kumekuwa na ubishi mkali kati ya Wizara ya Utumishi na Hazina kuhusu nyongeza ya mwaka huu iwe mpaka kiasi gani, nikaingilia kati nikakubaliana na utumishi, Hazina walikuwa wanataka ipingue kidogo,”  Wananchi waliunga mkono kusudio la Rais  la kutaka kukutana na waajiri katika sekta binafsi "Kuna malalamiko mengi tunayapokea kama serikali kutoka kwa wafanyakazi wa sekta binafsi ambayo kwakweli yanatuumiza, sina budi kukutana na waajiri ili tuzungumze kiundani kwa kutafuta ufumbuzi."
Pongezi kwa wafanyakazi wote kwa kuonyesha mshikamano katika maadhimisho ya Mei Mosi ya mwaka huu na kwamba kinachosubiriwa sasa ni utekelezaji wa majibu ya hoja za wafanyakazi.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom