Pages

Ijumaa, Mei 02, 2014

Simu za mkononi zinavyoweza kufahamisha mahala alipo mtumiaji


Tofauti na vifaa vya kiteknolojia kama vile kompyuta na tabiti (tablet), baadhi ya simu za kisasa zina uwezo wa kutoa taarifa za mahala mtu alipo au kilipo kitu fulani.
Hata hivyo, uwezo huu utokanao na maendeleo ya teknolojia ya dijitali unaelezwa kuwa na uzuri na ubaya wake.
Kwa mfano, watumiaji wa simu hizi wamekuwa wakijiuliza kuhusu masuala ya faragha kwa mhusika na hata usalama wa mahala alipo.

Tukirudi katika maudhui ya simu kutumika kujulisha mahala alipo mtu, kuna teknolojia kadhaa zinazotumiwa na watengenezaji wa simu katika kuhakikisha hilo linawezekana. Makala haya yataangazia baadhi ya teknolojia hizo.
Teknolojia ya GPS
GPS au kwa kirefu Global Positioning System ni mtambo wa satelaiti unaotambua na kuelekeza maeneo mbalimbali hapa duniani.
Mtambo huu unaoendeshwa na kitengo cha ulinzi cha Serikali ya Marekani, ulianza kutumiwa katika simu mwaka 1990. Teknolojia hii  inafanya kazi  saa 24  na ina uhakika wa kutoa muda halisi wa umbali fulani, umbali wa mahali kwenda mahali pengine pamoja na kutoa muda wa sehemu mbalimbali za dunia kwa wakati mmoja.
Aidha, teknolojia hii iliyopo katika simu za mikononi  inaweza kutumika kuonyesha kifaa kilipo ama kitakapokwenda
Baadhi ya Serikali duniani zimetengeneza mifumo yake ya GPS katika kutekeleza majukumu yao. Hata hivyo, mifumo hii inaelezwa kuwa haiingiliani na mfumo wa awali uliotengenezwa na Wamarekani.
Kwa mfano, Warusi mfumo wao wameupa jina la GLONASS, Japan wana Quasi-Zeneth, Ulaya kuna Galileo. India wana mfumo wa IRNSS. Wachina kwa upande wao wana  mfumo wao uliofanyiwa majaribio mwaka 2012.
Mwaka 2012 watalaamu wa utengenezaji simu za mkononi walikuwa katika mkakati wa kutengeneza ‘processor’  ya simu ambayo itakuwa na uwezo wa kutumia aina zote za mifumo hii inayowezesha kujua mahala alipo mtu au kilipo kitu. CHANZO MWANANCHI.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom