Pages

Ijumaa, Mei 02, 2014

MANENO MAZURI KATIKA CHANGAMOTO ZA MAISHA

"Kila mtu anao uwezo wa kufanikiwa, usiogope kuthubutu, kwani unapofanya jambo fulani kwaajili ya mafanikio, siku zote  hautakiwi kukata tamaa, mafanikio yapo kwa yule mwenye juhudi, na ambaye anaweza kupambana na changamoto bila kukata tamaa"
***********************************************************
"Siyo lazima uanze na kipato kikubwa katika kutafuta mafanikio kwani siku zote unaambiwa kile ulichonacho ukikitumia vizuri kinaweza kukamilisha ndoto zako jambo la msingi ni kuwa na nia madhubuti bila kukata tamaa, kwani siyo wote ambao wamefanikiwa walianza na kipato kikubwa"
***********************************************************
"Usichanganye kazi na mawazo potofu, kwani siyo kila anayekuona unataka kutimiza malengo yako atafurahi, ni vyema kuwa makini kwani yawezekana ukashindwa kutimiza malengo yako kutokana na vikwazo vya binadamu ambao wanatumia fursa ya kukurudisha nyuma ili ukate tamaa, kumbuka kumshirikisha Mungu katika kila jambo."

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom