Lengo ni kuwaepusha wanafunzi ambao ni watoto na janga la Ukimwi, pia ipo haja kuangalia kwanza umri wao na siyo kuwafundisha tu juu ya matumizi ya kondomu bila kuwagawa makundi kulingana na umri wao. Wanafunzi ambao wako madarasa ya chini waelimishwe kulingana na ukubwa na siyo vizuri kuanza kumfundisha mtoto jinsi ya kutumia kondomu wakati hajapevuka elimu hii haiwezi kumsaidia kwasababu hajui ngono ni nini.
Kwa vile tunataka kuwasaidia watoto wetu ili waepuke Ukimwi basi watafutwe waelimishaji rika ili watuambie ni mbinu gani tuzitumie kufikisha ujumbe wa Ukimwi kwa watoto wadogo ambao hawajafikia umri wa kujua mambo ya ngono. lakini zaidi ya hapa ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa tukidhani atacheza na kumbe ni kupoteza muda bure. Natambua kwamba watoto wadogo wanatakiwa kujua madhara yaletwayo na Ukimwi lakini siyo kuwafundisha matumizi ya kondomu. Na Dr Raphael Kalinga, Mkurugenzi Sera Mipango na Utafiti wa TACAIDS.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni