Pages

Jumamosi, Julai 12, 2014

ISOME HII KWA UMAKINI "RAFIKI NILIOSOMA NAO"

Baadhi ya marafiki niliosoma nao shule moja ama marafiki wa utotoni.
Wengine ni.
1. Wafanyakazi makampuni makubwa
2. Wanamiliki magari ya kifahari.
3. Wapo ulaya wanakula raha
4. Wanaendesha familia zao bila shaka
5. Wanawatunza wazazi wao vyema kabisa bila tatizo.

*Hawa wakanifanya nijisemee kuwa Mungu ana upendeleo... Kwanini raha ziwe kwa watu flani tu... Kwann shida ziwe kwangu mimi??
Mara nikaanza kukutana na marafiki wengine tuliosoma nao.
1. Wengine wamezikwa tayari.
2. Wengine walipata ajali na kupoteza viungo vyao.
3. Wengine ni wagumba
4. Wengine wanalala njaa na hata kesho yao hawaijui.
5. Wengine ni yatima.
6. Wengne mwaka wa nne huu wanazurura hawajapata kazi.
7. Wengine ni wagonjwa mahututi....
**Baada ya ushuhuda huu nikajiona mimi ninayo nafuu sana... Na hapo nikatambua ewe Mungu hauna upendeleo... Haya magumu tunayopitia ni mapito tu na haimaanishi kuwa Mungu ana upendeleo... Hakuna aliye na haki zaidi ya mwenzake mbele ya Mungu.. Nd'o maana sote tunazaliwa kwa namna moja na hata kufa kwetu ni aina ileile.......
**Asante Mungu kwa sababu wewe ni mwema wakati wote 
NA:George Iron Mosenya

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom