Pages

Alhamisi, Septemba 25, 2014

HONGERA SANA KWA BLOG YETU IMETIMIZA MIAKA 4 TANGU KUANZISHWA KWAKE.

Kwanza ningependa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa nguvu, na kipaji cha utunzi, pia nawashukuru wadau wote ambao tumekuwa pamoja katika blog hii. Tokea tulipoanza hadi leo hii natimiza miaka minne, nimekuwa nikiweka simulizi pamoja na mada mbalimbali za kuelimisha jamii, nashukuru Mungu kwa kiasi kikubwa nimepata wadau wengi ambao wamependa kile ninachokifanya, lakini pia na mimi nimeweza kujifunza na kufanya mambo mengi kupitia kazi yangu ya blog, kwani kupitia blog hii nimeweza kufungua  kampuni ya Della Media Production Ltd.

 Kupitia kampuni yangu natarajia kutoa vitabu vingi zaidi pamoja na kuwasaidia vijana ambao ni waandishi wazuri wa vitabu vya simulizi za maisha, kuweza kufikisha ujumbe wao katika jamii. Mbali na yote hayo ni kufanya kazi za utengenezaji wa matangazo mbalimbali ya biashara ambayo nimekuwa nikifanya. Nawashukuru sana kwani nia nilikuwa nayo njia nimeipata tangia nimeanza kazi ya blog na sasa mtaendelea kupata mambo mazuri sana zaidi kupitia blog ikiwa lengo ni kuelimisha jamii kupitia kusoma simulizi na mada mbalimbali zinazoelimisha jamii. ASANTENI SANA TENA SANA NAWAPENDA SANA TUENDELEE KUWA PAMOJA.

Maoni 5 :

Bila jina alisema ...

Hongera sana Adela mimi ni mdau wako wa muda mrefu ukweli ni kwamba nimejifunza sana mambo mengi kupitia blog hii.

Bila jina alisema ...

Hongera sana endelea kutuletea simulizi motomoto

Amor alisema ...

HONGERA sana Adela. Mimi nakupenda sana. Una upeo mkubwa na sauti tamu sana. Kazana ili ujulikane pia kimataifa Afrika na duniani kote. Usiruhusu mtu akwambie huwezi na usijidharau hata kidogo. Una kipaji mama. Kazana na baraka zikutawale!

Bila jina alisema ...

Hongera my dear be blessed

Adela Kavishe alisema ...

Asanteni sana wadau tuendelee kuwa pamoja nawapenda sana

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom