Pages

Jumatatu, Novemba 24, 2014

MANENO MAZURI KWA WAPENDANAO"Mwendo wako unanikosha sana mpenzi, sauti yako ndiyo usiseme, una sauti nzuri sana ambayo inaweza kumtoa nyoka pangoni, ama kweli wewe ni kila kitu kwangu, mbali na uzuri ulionao, tabia yako ni nzuri sana nakupenda mpenzi wangu  Mungu atujalie tupendane milele."
 **********************************************************
"Nilalapo nakuwaza wewe, niamkapo natamani nikuone ukiwa karibu yangu, ewe barafu wa moyo wangu usikae mbali nami, nakosa raha ukiwa mbali nami, nafarijika uwapo karibu yangu fahamu kuwa nakupenda sana na wewe ni faraja ya maisha yangu"
 ********************************************************
"Mapenzi yangu kwako ni zaidi vile unavyofikiria mpenzi, nakupenda sana, nafurahi na wewe unanipenda na kunijali yaani mahaba unayonipa, hadi mimi mwenyewe naogopa wakati mwingine najionea wivu mwenyewe, asante mpenzi  nakuomba tupendane milele daima."


Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom