Waziri Mkuu Mizengo Pinda ameitaka CCM kupitisha majina ya wagombea wa nafasi ya urais, ubunge na udiwani kwa kuzingatia matakwa ya wananchi ili kuepuka chama kupoteza nafasi kwa jamii.
Alionya kama chama kitapuuza matakwa wananchi, kinaweza kupata pigo kama ilivyotokea katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2010 katika Jimbo la Iringa na majimbo mengine kadhaa nchini.
“Mimi ni mlezi wa Mkoa wa Iringa kichama, nawaombeni wekeni masilahi ya chama mbele badala ya masilahi ya mtu binafsi na mnapokwenda kutafuta viongozi wa ngazi ya kata, jimbo na urais. Hakikisheni wagombea mnaowaleta ni wale wanaokubalika na jamii ya eneo husika,” alisema Pinda.
Uchaguzi Mkuu ujao, Dk Asha Rose Migiro amewataka wana CCM kuwa wamoja ili kukiletea chama ushindi na kuacha kugawanyika miongoni mwao.
“Kama tukiwa wamoja, hatuna kitakachotushinda bali tutafanya vizuri na kwa umoja wetu tutashinda kuanzia udiwani, ubunge hadi urais,” alisema. Waziri huyo ambaye hakuonekana kujipigia debe kama wafanyavyo wengine, mbali ya kutotumia lugha ya kejeli kwa wagombea wenzake, muda mwingi aliutumia kuisifu Serikali ya awamu ya nne na kuwa makini katika kauli zake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni