Jumamosi, Juni 20, 2015

"Sifa nyingi bila vitendo ni sawasawa na bure"


Katika maisha unapojibebesha mambo mengi makubwa ipo siku unaweza kuwa na  shida lakini usimpate mtu wa kukusaidia, mfano mtu ambaye anajigamba sana kuwa ana uwezo mkubwa katika mambo mbalimbali lakini kumbe hana chochote ila anataka watu wajue kuwa anacho, wapo vijana ambao wamekuwa wakikosa wachumba kutokana na kuwa majigambo , kujifanya kuwa anamiliki vitu vikubwa na utajiri mkubwa ilihali ni uongo mwishowe anashindwa kumpeleka mchumba wake kwake ama kwao, kutokana na hofu kuwa kile alichokuwa anajigamba hakipo.

 Ni vyema mtu ukawa mkweli kuliko kusema uongo mfanye mtu akukubali jinsi ulivyo na si vinginevyo. Wakati mwingine mtu unaweza kukosa msaada kwa kujifanya unacho kumbe huna, yaani unaweza kukosa mambo mengi ambayo yangekusaidia kukutoa katika umasikini  kutokana na kuwa na sifa zisizokuwa na maana hivyo hata zikitokea fursa watu wanashindwa kukushirikisha huku wakijua kuwa wewe hauna shida, kumbe unamatatizo kibao ila unajifanya hauna matatizo. kumbuka majigambo kibao hayana maana kama hauna kitu na mficha maradhi sikuzote kifo umuumbua.

Maoni 2 :

Bila jina alisema ...

NI KWELI ADELA NA HII NI TABIA YETU WATANZANIA MADHANI NISEME WAAFRIKA .MTU HANA ANAJISIFIA MPK INANIUZI NA HATA ALIYENACHO ANATAKA KUJIONESHA ULIMWENGU UMJUE .KWA MTAZAMO WANGU NI USHAMBA KWA WALIONACHO NA KUJIONESHA KAMA UNACHO NI CHAKO . NA KWA WASIONACHO WAKATI MWINGINE NI VIGUMU KUONESHA HAWANA KWANI TUNASAIDIANA NA KUKASHIFIANA ,KUSEMANA ,KUTANGAZIANA NDO UNAKUTA ASONACHO ANAKUWA MUOGA KUSEMA HANA KUHOFIA KUSEMWA.
MUNGU AMBARIKI KILA MTU AWE NACHO JAPO KIDOGO CHA KUMKIDHI MAISHA

ADELA KAVISHE alisema ...

tuko pamoja san mdau jambo la msingi ni kujitambua, na kujikubali katika maisha yetu ya kila siku.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom