Pages

Jumatatu, Julai 27, 2015

" Hivi ndivyo alivyojibu swali linalohusu suala la Ushoga na Usagaji" Obama katika ziara yake nchini Kenya.

Akijibu swali linalohusu suala la ushoga na usagaji kutoka kwa muandishi wa habari,  Rais wa Marekani Obama aliitaka Serikali ya Kenya kuwatambua  na kutowanyanyasa wale wote wenye mapenzi na uhusiano wa jinsia moja. "Nikiwa kama Mmarekani mwenye asili ya Africa, natambua athari za kubaguliwa, endapo tatizo hilo litapewa nafasi eti kwa kuwa fulani yuko tofauti, ndipo suala la uhuru linapoanza kwenda mrama na mambo mabaya kuanza kujitokeza"Alisisitiza.

Hata hivyo hapohapo Rais wa Kenya, Kenyata alipinga ushauri huo wa kuhamasisha uhusiano wa jinsia moja nakusema"Lazima tuwe wakweli katika baadhi ya mambo, Wakenya na Wamarekani wanashirikiana katika mambo mengi kama vile ujasiriamali, demokrasia na masuala ya kifamilia, lakini mambo mengine kiukweli si sehemu ya tamaduni na dini zetu alisema Kenyata.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom