“Uamuzi mgumu na si jambo dogo, tena ni zito ambalo halihitaji majibu
mepesi kuhusu kuondoka kwa Lowassa CCM na kujiunga Chadema...kwangu bado
nayatafakari yale yaliyotokea Dodoma kwa sababu waziri huyo aliwekeza
sana ndani ya chama kilichomlea na kumkuza tangu akiwa kijana,” alisema
Mgeja.
alisema kila mmoja aliguswa kuondoka kwa Lowassa CCM na kwenda Chadema
ambacho ni chama kikuu cha upinzani nchini kwa sasa.
Hata hivyo, alisema mambo yaliyotokea katika mkutano wa kuteua mtu atakayewania kiti cha Rais kwa tiketi ya CCM mkoani Dodoma, yanatakiwa waachiwe wana CCM wenyewe wayazungumze katika vikao vyao vya ndani kuliko kuzungumzia nje.
“Tulimzoeya sana, tumesikitika na wengi tunaamini tumemkosa ndani ya chama ila kwangu bado mwanachama na kiongozi wa CCM bali tuendelee kutafakari yaliyotokea huko na tuyajadili ndani ya vikao,”
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga, ambaye pia ni mwenyekiti wa Mzalendo foundation, Khamis Mgeja, akisisitiza kitendo cha Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, kuhama chama hicho na kujiunga Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) si jambo dogo na la kutolea majibu mepesi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni