Jumamosi, Januari 02, 2016

UNAWEZA KUWA UMEPENDWA LAKINI WEWE HUJAPENDA.


Waswahili husema mpende akupendaye asiyekupenda achana naye lakini, pia unaweza kupendwa na wewe haujapenda, na pia ni muhimu kupenda unapopendwa, wakati mwingine unaweza kupenda lakini unayempenda hakupendi, sasa ni bora kumpenda anayekupenda. 

Kuna baadhi ya watu hujikuta katika mahusiano ya kulazimisha, yaani unampenda mtu ambaye hajui thamani ya pendo lako mwisho wa siku unabaki ukiumia wewe na mwenzio akiona ni jambo la kawaida, kwasababu hakupendi ila anajilazimisha tu kuwa karibu yako kutokana na sababu fulani, labda anakuonea huruma anahisi akikuacha utajinyonga au anajiweka kutokana na mali ulizonazo, kwahiyo ni muhimu kuwa makini kwani mapenzi hayatabiriki.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom