Pages

Alhamisi, Februari 25, 2016

Mazungumzo ya wapendanao "Je kweli unanipenda?"

RUBY: Unajua nakupenda sana Mume wangu yaani nakupenda najisikia furaha sana ukiwa karibu yangu kila wakati.
JOHN: Asante sana Mke wangu usijali tuko pamoja.
RUBY:Ila mume wangu, kuna kitu kinanisumbua moyoni, ni bora tu nikueleze ukweli.
JOHN: Mmmh jambo gani tena linakusumbua, embu nieleze"
RUBY: Maranyingi nimekuwa nikikutamkia kuwa nakupenda sana, lakini sijawahi kukusikia wewe ukinitamkia kuwa unanipenda, Je kweli unanipenda?"
JOHN: Hahahaha wanawake bwana, sasa mimi na wewe hadi tunaishi pamoja, inamaana hujui kama mimi nakupenda, acha mambo yako bwana mimi sioni kama hilo ni tatizo.
RUBY: Usiseme hivyo John mimi natamani na napenda uwe unanitamkia maneno mazuri  ni faraja sana kwangu kwasababu nakupenda"
JOHN: Haya mke wangu nakupenda sana, usijali wewe ni kila kitu kwangu sawa mama.
RUBY:Nakupenda pia mume wangu tupendane milele.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom