Pages

Alhamisi, Machi 17, 2016

MANENO MAZURI KUTOKA KWA DINA MARIOSKuna wakati ADUI yangu alidhamiria kunifanya kichekesho,kuniaibisha,kunifedhehesha, kuiua nafsi yangu,kuipoteza thamani yangu,niwe kituko nisiwe wa wakutumainiwa wala kutegemewa,watu waninyooshee vidole,kufinyana kwa umbea kuniteta na kunicheka.

Nilitambua mimi mwenyewe siwezi kupambana na adui yangu.Nikamgeukia Mungu nikamuomba yeye ndio apigane vita hiyo.Na kama yeye alimruhusu ADUI anifedheheshe basi aonekane katika maisha yangu kama alivyoonekana kwa Yusuf lile alilopanga katika maisha adui asiwe na mamlaka ya kuliharibu.


Nikamwambia Mungu wangu utete nao wanaoteta nami,Upigane nao wanaopigana nami.Uishike ngao na kigao usimame unisaidie waaibishwe, wafedheheshwe wote wanaoitafuta nafsi yangu.
Kupitia yeye nilipata Amani ya moyo wangu huku nikaamini Yatakwisha.
Napenda nikwambie leo wale wote wanaoichimbia shimo nafsi yako shimo hilo wataingia wenyewe.
Wale wote wanaokusagia maneno na kuligeuza jina lako chakula.Wanakunenea kushindwa,laana,mikosi,ipo siku watayameza maneno yao wenyewe.Tena wanaapizana tutaona kama atafanikiwa kama walivyoapizana ndivyo watakavyoaibika.
Shimo walilochimba kwa kazi yako,biashara zako,familia yako,afya yako,jina lako...Shimo hilo litawafukia wenyewe.
Wewe endelea kumtumainia aliye juu.


‪#‎zaburi35‬ ‪#‎maishaclass‬

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom