Jumatatu, Novemba 22, 2010

Wanaume nchini wametakiwa kuacha kuona aibu wanapotendewa ukatili na wake zao majumbani.

Mwito huo umetolewa jijini Mwanza na mtandao wa polisi wanawake  wanaokaa dawati la kijinsia walipokuwa katika semina ya siku mbili iliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Acord  linaloshughulika na mambo ya jamii likiwemo la usawa wa kijinsia kwa wanawake na wanaume. Polisi hao wamesema ukatili wa kijinsia sio kwa wanawake tu wapo na wanawake ambao wanafanya ukatili kwa waume zao. wamesema kwakuwa wanaume wamejenga dhana kwamba ni aibu mwanamume kupigwa na mwanamke, hujikuta wakilazimika kuteseka kwa kuona aibu kwenda kutoa taarifa mahali ambapo wangepatiwa msaada.


Tazama pichani mwanamke akimbamiza mwanamume,, wanaume wanaofanyiwa ukatili na wake zao wapo  na chanzo mara nyingi ikiwa ni wivu wa kimapenzi,migogoro,na dharau. inawezekana kuna siri nyingi sana katika baadhi ya ndoa za waliowengi. MAPENZI NI KUPENDANA,KUJALI, NA KUHESHIMIANA NA SI KUFANYIANA UKATILI.


Maoni 3 :

Yasinta Ngonyani alisema ...

nanukuu:- "MAPENZI NI KUPENDANA,KUJALI, NA KUHESHIMIANA NA SI KUFANYIANA UKATILI." nimeupenda huu msomo Adela. Ni kweli kabisa kuna wanaume wanaoteswa pia.


ADELA KAVISHE alisema ...

@Yasinta tuko pamoja wangu

emu-three alisema ...

Duh jamani, hivi kwanini kuwe na hali hiyo `ukatili' ili iweje, mtu anapata faida gani? sijui..Adela, tupo pamoja mpendwa!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom